} });
 

 

Mkuu wa Wilaya ya Magu mkoani Mwanza, Salum Kalii, ameagiza Mwalimu Martin Mambosasa, wa shule ya msingi Ilungu anayetuhumiwa kuwadhalilisha kingono na kuwafanyia michezo michafu wanafunzi wawili kwenye kitanda kimoja kwa muda wa miaka saba kuondolewa Wilayani humo.

Agizo hilo amelitoa kwenye kongamano la kuweka mikakati ya kukabiliana na ongezeko la vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, mimba na ndoa za umri mdogo, utoro kwa wanafunzi ili kuongeza ufaulu na ndipo alipotoa maelekezo hayo.

“Kesi ambazo tulizibaini ikiwepo Mwalimu mmoja anayeitwa Mambosasa tulimkamata akiwa na mahusiano na wanafunzi zaidi ya watatu, na wakati mwingine alikuwa anawalaza kwenye kitanda kimoja wote wawili na kuwafanyia mambo ya ajabu sana, nimesema mimi simtaki kwenye wilaya yangu” DC Kalii.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top