} });
 


MWAMUZI wa mchezo kati ya Simba na Yanga, Emmanuel Mwandembwa, ni mali ya Yanga kutokana na michezo yote ya Yanga aliyoichezesha timu hiyo kuondoka na pointi zote tatu, huku Simba wakishindwa.

 

Mwandembwa ameonekana kumudu presha ya michezo mikubwa kwa msimu huu na kuchaguliwa kusimamia mchezo huo ambao utapigwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar.

 

Waamuzi wengine watakaomsaidia Mwandembwa katika mchezo huo ni Frank Komba, Hamdani Saidi, na Ramadhan Kayoko.


Takwimu zinaonyesha kuwa mwamuzi huyo amechezesha mechi mbili za Yanga, dhidi ya Azam na Biashara United ambapo Yanga waliibuka na ushindi wa bao 1-0 katika kila mchezo.

 

Katika michezo ya Simba aliyochezesha msimu huu, Mwandembwa ilikuwa dhidi ya Tanzania Prisons (1-1) na Dodoma Jiji (3-1).

 

Katika michezo aliyochezesha mwamuzi huyo kwa msimu huu Simba imevuna pointi nne huku Yanga wakifanikiwa kuchukua zote sita na hivyo takwimu zinaonyesha kuwa ana bahati zaidi na Yanga.

 

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi, Soud Abdi, akizungumza kabla waamuzi hao hawajatajwa alisema: “Katika mchakato wa kumtafuta mwamuzi wa mchezo huo, tunaangalia ni yupi alikuwa na mwenendo mzuri kwa siku za karibuni.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top