} });
 

 

Mahakama ya Kitamaduni nchini Zimbabwe yamtaka Mke wa rais wa zamani wa Zimbabwe, Grace Mugabe kufika mahakamani hapo kwa tuhuma za kufanya mazishi “yasiyofaa” ya hayati Rais Robert Mugabe.

Grace Mugabe anatuhumiwa kwa kwenda kinyume na utamaduni wa jamii yao kwa kumzika Mume wake katika boma la familia badala ya kumzika sehemu iliyochaguliwa na jamaa zake na mama yake.

Katika waraka kutoka kwa Chifu Zvimba, ambaye ni mkuu wa kitamaduni wa nyumbani kwa kina Mugabe amesema Grace anatakiwa kuufukua mwili wa hayati Rais Mugabe ili uzikwe tena kulingana na utamaduni wa watu wa Zvimba.

Pia ameagizwa kulipa faini ya ng’ombe na mbuzi kwa kukiuka utamaduni. Mugabe alifariki mwaka 2019 katika hospitali moja nchini Singapore akiwa na umri wa miaka 95.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top