} });
 


Kenya imepiga marufuku safari zote kutoka Somalia bila kutaja sababu ya hatua hiyo. Mkurugenzi wa Mamlaka ya Anga amesema maelekezo yalitoka Serikalini.

Mamlaka ya Anga imesema ndege za dharura za kitabibu na walio na ujumbe wa masuala ya kibinadamu ya UN zitaruhusiwa kuingia.

Kenya na Somalia zimekuwa na mzozo wa mpaka baharini tangu mwaka 2014, wakati Mogadishu ilipopeleka kesi dhidi ya Kenya katika Mahakama ya Kimataifa ICJ.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top