} });
 

 

Queen wa Pop ambae pia ni Mshindi wa Tuzo za Grammy mara tano Janet Jackson ameamua kuzipiga mnada nguo zake zaidi ya elfu moja ikiwa ni sehemu ya kusherehekea miaka 55 ya kuzaliwa kwake ambapo mnada huo unafanyika Jijini New York Marekani.

Moja ya nguo zitakazouzwa ni lile sweta alilolivaa kwenye video ya ‘scream’ na ile kofia ya baseball aliyoivaa kwenye video ya “Rhythm Nation” ambapo pesa inayotarajiwa kukusanywa inafika Dola za kimarekani Milioni 2.

Imewekwa wazi kwamba sehemu ya pesa itayopatikana itapelekwa kusaidia Watoto kote duniani kupitia Taasisi ya Compassion International ambayo hufanya kazi na Makanisa mbalimbali kusaidia Watoto kiroho, kiuchumi, kijamii na kuwakwamua kutoka kwenye umasikini.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top