} });
 


Wachezaji wa Simba, Joash Onyango na Taddeo Lwanga wameanza mazoezi na wachezaji wenzao baada ya hali zao kiafya kuimarika baada ya kupata majeraha katika mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs ulichezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Katika mchezo ambao Simba walishinda mabao 3-0, Onyango na Lwanga walishindwa kumaliza mechi kutokana na kugongana vichwa.

Daktari wa timu hiyo, Yassin Gembe amesema hali za nyota hao zinaendelea vizuri na ndiyo sababu ya kuwaruhusu kufanya mazoezi ingawa wanaendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari.

“Onyango na Taddeo wameanza mazoezi na wenzao leo hali zao zinaendelea vizuri kabisa lakini tunaendelea kuwaweka chini ya uangalizi wa madaktari ili wasipate maumivu mengine,” Gembe.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top