} });
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Mei 19, 2021, amefanya mabadiliko ya wakuu wa mikoa miwili aliowateua hivi karibuni. 

David Kafulila anakwenda kuwa mkuu wa mkoa wa Simiyu badala ya Arusha kama alivyoteuliwa awali, akichukua nafasi ya John Mongella 

Aidha Rais Samia amembadilisha John Mongella kutoka kuwa Mkuu wa mkoa wa Simiyu na kwenda kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha. Kabla ya kuteuliwa kwenda Simiyu Mongella alikuwa mkuu wa mkoa wa Mwanza.

Rais Samia amesema sababu ya mabadiliko hayo ni uzoefu wa Mongella kuongoza jiji la Mwanza hivyo inabidi akaongoze jiji la Arusha ili Kafulila ambaye ndio anashika nafasi hiyo kwa mara ya kwanza aanzie Simiyu.

Mabadiliko hayo ameyafanya wakati akitoa hotuba baada ya kuwaapisha wakuu wa mikoa wateule na wakuu wa taasisi mbalimbali, Ikulu Dar es salaam.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top