} });
 

 

Kutoka Ikulu Chamwino Dodoma Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa viongozi 3.

Taarifa iliyotolewa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Athman Kattanga imeeleza kuwa uteuzi wa viongozi hao umetenguliwa kuanzia tarehe 30 Aprili, 2021.

Kwanza, Rais Samia ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASACProf. Tadeo Andrew Satta. Sambamba na hatua hiyo, Rais Samia pia ametengua uteuzi wa wajumbe 6 wa bodi ya TASAC.

Pili, Rais Samia ametengua uteuzi wa Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Hassan Mwang’ombe.

Tatu, Rais Samia ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania Dkt. Harun Kondo.

Sambamba na hatua hiyo, Rais Samia pia amevunja Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top