} });
 


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla amemaliza sintofahamu ya uongozi wa manispaa iliyojitokeza Kati ya Meya wa Manispaa ya kinondoni, Songoro Mnyonge na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Spora Liana.

Utatuzi wa mgogoro huo umefanyika leo katika kikao cha pamoja kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa na kuwakutanisha Meya na Mkurugenz wa Manispaa ya Kinondoni.

Makalla amewataka Viongozi hao kurejea ofisini na kufanya kazi kwa pamoja, kutekeleza miradi ya maendeleo na kutatua kero za Wananchi.

Kwa upande wa Meya na Mkurugenzi wamemaliza tofauti zao na wamehaidi kufanya kazi kwa pamoja kwa maslahi mapana ya Wananchi.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top