} });
 


Ikiwa tayari ni wiki moja imepita baada ya wanandoa matajiri zaidi duniani, Bill Gates na mkewe Melinda Gates kutangaza kupitia ukurasa wa Twitter kwamba penzi lao limefika mwisho, imebainika kwamba kumbe mwanamke huyo alianza mchakato wa kudai talaka tangu 2019.

Kwa mujibu wa Daily Mail, gazeti la nchini Uingereza, limefichua kwamba linao ushahidi wa madai hayo na hatua hiyo ilichukuliwa na Melinda kutokana na ukaribu wenye kutia shaka kati ya mumewe na mfanyabiashara mwingine mkubwa, Jeffrey Epstein ambaye kwa sasa ni marehemu.

Inaelezwa kwamba, Melinda aliwahi kunukuliwa na Jarida la Wall Street Journal mwaka 2019 akieleza kuwa ndoa yao ilikuwa ikielekea kuvunjika na tangu kipindi hicho, amekuwa akishirikiana na wanasheria wake wakiongozwa na Robert Stephan Cohen kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa katika mchakato wa kupeana talaka.

Ukaribu wa Bill Gates na Epstein ulianza mwaka 2013 na inaelezwa kuwa mkewe hakuwa akifurahia ukaribu wao na alishamuonya mumewe mara kadhaa, hasa ikizingatiwa kwamba Epstein amewahi kutumikia kifungo gerezani kwa makosa ya udhalilishaji wa watoto kingono.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top