Na Nicholaus Paul Lyankando - Geita
Shirika la viwango Tanzania TBS Kanda ya Ziwa limewataka wauzaji na wakulima pamoja wajasiliamali mkoani geita kuhakikisha bidhaa zao zinakaguliwa na shirika hilo ili zikubalike katika nchi za nje.
Hayo yamesemwa na meneja wa shirika la viwango Tanzania kanda ya ziwa Joseph Ismail wakati utoaji wa mafunzo ya namna ya kuwawezesha wauzaji wa bidhaa mbalimbali pamoja na wakulima wa mchele mkoani humo ili kuzalisha mchele wenye viwango na usalama kwa watumiaji.
“Naamini, wengine yamkini walikuwa hawafanyi kwa sababu hawana elimu. Kwa hiyo nina amini baada ya elimu hii na baada ya udadavuaji ambao tutakuwa tumewapa nina amini asilimia kubwa ya wananchi au wasindikaji watapata leseni za ubora na itawaongezea confidence ya kufanya ndani na nje ya nchi ” Joseph Ismail
Aidha, Mkuu wa wilaya ya Geita Fadhili Juma
ameshukuru shirika la viwango TBS kufanya mafunzo wilayani geita kwani geita
ndo inaongoza kwa kulima mpunga kwa wingi na kuomba wauzaji pamoja na wakulima
kutumia mafunzo hayo waliyoyapata katika kujinufaisha kwa kupata masoko ya
kimataifa
“Tunashukuru kama Serikali tumepokea hayo mafunzo kwa mikono yote kwa sababu ni mafunzo ambayo yanakuja na tija, wanapewa mafunzo wale wajasiriamali au wachakataji wa zao la mpunga ili kupata mchele.”
Kwa upande wao wasambaji wauzaji na wakulima walioshiriki mafunzo hayo wamelishukuru shirika la viwango Tanzania TBS kanda ya ziwa kwa kufanya mafunzo hayo pia wamewaomba waendelee kutoa elimu ya mara kwa mara ili kuendeleza sera ya Tanzania ya viwanda.
Post a Comment