} });
 


Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameagiza kuvunjwa kwa Jumuiya ya Maji Kijiji cha Berege Wilayani Mpwapwa huku akitoa onyo la ubadhilifu wa fedha za jumuiya ya watumia maji katika mradi wa maji kwenye  kijiji hicho.

Ametoa kauli hiyo wakati wa  ziara yake ya kukagua utekelezaji na uendeshaji wa miradi ya maji pamoja na kuzungumza na wananchi wa kijiji hicho kilichopo halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mkoa wa Dodoma.

Waziri Aweso alipokea malalamiko ya wananchi kuhusu  jumuiya ya watumiaji maji kuwa fedha zinakusanywa lakini hazipelekwi benki.

Amebainisha kuwa jumuiya za watumia maji nchini zina changamoto kwenye usimamizi wa miradi na matumizi sahihi ya makusanyo ya fedha.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top