} });
 

 

Hali ya sintofahamu imezuka kwa wakazi wa kijiji Cha Nguyami Kata ya Idibo wilaya ya Gairo mkoa wa Morogoro baada ya kaburi la mwili wa marehemu Rehema Michael (35) kukutwa umefukiliwa na kukatawa baadhi ya viungo vya mwili huo ikiwemo kichwa, sehemu za Siri na moyo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Gairo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya, Siriel Nchembe amesema marehemu huyo alifariki baada ya kugongwa na gari na amezikwa mei 23 mwaka huu Katika kijiji hicho na muda mchache badae watu wasiojulikana walifika Katika kaburi hilo na kufukua Kisha kuondoa baadhi ya viongo vya mwili.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top