} });
 


Mbunge wa Viti Maalum  (CCM),  Hawa Mchafu amedai baadhi ya wanaume wa Tanzania wanatumia nguvu kubwa kujadili habari za Simba na Yanga kuliko hata kujadili afya zao.

Hawa amesema kama nguvu hiyo ingetumika kujadili masuala ya afya ikiwemo kupima UKIMWI  huenda vita dhidi ya ugonjwa huo ingekuwa nyepesi.

Mbunge huyo ametoa kauli hiyo leo May 11, 2021  bungeni Dodoma wakati akichangia  hotuba ya bajeti ya Wizara ya Afya mwaka 2021/22.

“Wanaume ile nguvu mnayoitumia kujadili Simba na Yanga, Siasa na uke wenza ihamisheni ipelekeni kwenye masuala ya kupima virusi vya UKIMWI” Mchafu

Kuhusu ukeketaji, amesema wanaume wanatakiwa kutangaza hadharani kwamba hawawezi kuwaoa wanawake waliokeketwa lakini kukaa kwao kimya bado ukatili huo utaendelea.

Kwa mujibu wa Mbunge Hawa, wanaume wakisema ladha ya waliokeketwa ni tofauti na wasiokeketwa, jambo hilo litakwisha mara moja na kubaki historia.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top