} });
 

 

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linawashikilia watu 161 wanaotuhumiwa kuhusika na wizi wa magari, pikipiki na vipuri vyake, katika oparesheni maalum iliyofanyika kuanzia April 26, 2021 hadi Mei 2.

 

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, amesema miongoni mwa waliokamatwa, wapo watuhumiwa watano ambao wanatajwa kuwa vinara wa wizi huo, waliokamatwa visiwani Zanzibar wakiwa na pikipiki 40 zinazodhaniwa kuwa za wizi.

 

Pia Kamanda Mambosasa ameeleza kwamba jeshi hilo limefanikiwa kuyapata magari mawili, Toyota Noah lenye namba za usajili T770 ACY na Toyota IST yenye namba za usajili T137 DMM sambamba na pikipiki 91, Bajaj 4 na vifaa vingine zikiwemo simu za mkononi, runinga, vipuri vya magari, mabelo ya nguo za mitumba na bastola moja aina ya Browning, vyote vikiwa vimeibwa katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Pwani.


soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top