} });
 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa kitabu cha maisha ya Mzee Mwinyi, alichokizindua kinafundisha mambo mengi ikiwemo la binadamu kupendana na si vyema kumfanyia mtu ubaya sababu hauwezi kujua kesho atakuwa nani.

“Mzee Mwinyi anatufundisha umuhimu wa sisi binadamu hususani viongozi kupendana na kushirikiana, mwaka 1981 aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, baada ya uteuzi huo alitakiwa kuhama nyumba ambayo ilipangiwa kukaa Waziri mwingine, Waziri mpya alikuja nyumbani na kumtaka aondoke haraka hata bila kumpa nafasi ya kuhamisha vitu vyake vya ujenzi Mzee Mwinyi aliondoka” Rais samia

“Baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na kufanyiwa vitimbwi hivyo vyote Mzee Mwinyi, alimteua Waziri huyo  kwenye Baraza lake la Mawaziri, sasa ndugu zangu kama huyo Waziri bado anaishi sijui anajisikiaje huko aliko”,  Rais Samia.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top