} });
 

 

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, ametoa uhuru wa kibiashara kwa wawekezaji wa Tanzania kuwekeza nchini Kenya bila kuwa na visa za biashara wala kibali cha kazi na kuwasihi wahakikishe wanazingatia sheria na kanuni zinazofuatwa na wawekezaji wa Kenya.

Kauli hiyo ameitoa May 5,2021 nchini Kenya wakati wa ufunguzi wa kongamano la wafanyabiashara wa Kenya na Tanzania ambalo wamelifungua kwa pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, na kuongeza kuwa watahakikisha wanarahisisha njia zote za ufanyaji biashara.

“Tungependa kuona wawekezaji wengi wa Tanzania waje wafanye kazi zao hapa Kenya, wawekezaji wa Tanzania mjue kwamba mko na uhuru wa kuleta na kufanya biashara zenu hapa bila kuombwa ‘business visa’ na work permits’ ila mfuate sheria na kanuni zilizowekwa na zile ambazo wenzenu wa Kenya pia lazima wazifuate” Rais Kenyatta

“Tuko na nafasi na nia ya kuhakikisha kwamba tukifanya pamoja tunaweza kuinua uchumi wa Tanzania na Kenya, naamini Mh Rais Samia Suluhu, kwa dhati ya kwamba tukiingia kwa njia ya kushirikiana ushindi utakuwa wa wananchi wa nchi zetu” Rais Kenyatta

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top