} });
 

 

Na Imani Anyigulile

Wananchi wa kata ya galula wilayani Songwe mkoani Songwe wameiomba serikali kulitafutia ufumbuzi ujenzi wa daraja la Galula ambalo limekuwa likiwa shinda wakandalasi.

Ujenzi wa daraja hilo ulianza katika awamu ya nne ya utawala wa Dkt. Jakaya Kikwete na umeendelea kujenmgwa katika awamu tano ya hayati Dkt. John Pombe Magufuli ujenzi ambao licha ya kujengwa kwa kingo na nguzo hatima ya kukamilika kwake bado haijulikani.

Wananchi hao wamesema kuwa kuna baadhi ya viongozi wamekuwa wakiwaahidi kujenga daraja lakini hawajaona kinacho endelea katika daraja hilo. 

Erasto Mpemba ni mwenyekiti wa kijiji cha galula amekiri kuwepo kwa ubovu wa daraja hilo na kueleza kuwa hakuna mweleo wowote wa kujengwa kwa daraja hilo. 

Naye afisa mtendaji wa kata ya Galula Anania Samweli amesema kuwa daraja hilo limekuwa likiwasumbua kwa muda mrefu lakini wakandarasi wamefanya jitihada za matengenezo lakini bado hakuna mafanikio.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top