} });
 

 

Familia katika kijiji cha Ebunyang’anyi kata ya Bunyala, Kakamega nchini Kenya imepatwa na mshtuko baada ya kuamka na kukuta jeneza lililokuwa na misalaba mitatu likiwa limewekwa mlangoni  nje ya mlango wa nyumba ya Peter Wekondi, mzee mkongwe ambaye pia ni mgonjwa.

Mmoja wa walioshuhudia kisa hicho cha kushangaza, Janepher Masika amesema kuwa jeneza hilo lilikuwa limefungwa kwenye kitambaa cheupe huku nzi wakiwa wamejaa juu yake.

 “Nilipokuwa nikienda shambani niliona jeneza nje ya nyumba ya majirani zangu na nikawaamsha kuwaarifu. Nilishtuka kwa sababu sijawahi kuona kitu kama hicho maishani,” Masika.

Kwa muda mfupi, tukio hilo lilikuwa limevuta umati mkubwa uliokusanyika katika nyumba hiyo kushuhudia kisa hicho kilichowaacha midomo wazi.

Baada ya kufungua jeneza hilo wenyeji hao waliachwa na mshtuko baada ya kupata mchanga na vifaa vingine visivyojulikana. Baadhi yao walikihusisha kisa hicho na ushirikina ambao walisema huenda mhusika alichukua hatua hiyo kutokana na wivu.

Jotham Makokha, mzee wa ‘nyumba kumi’ alitoa wito kwa wenyeji kupendana na kuishi kwa amani na uwiano.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top