} });
 


Mahakama ya Kikatiba nchini Afrika Kusini leo Juni 29, 2021 imemuhukumu Rais Mstaafu Jacob Zuma kifungo cha miezi 15, kwa kosa la kudharau mahakama.


Hii ni baada ya Korti ya Katiba kumpata na hatia ya kukaidi agizo la kufika mahakamani baada yakukosa kufika kwenye kikao cha uchunguzi wa kesi ya ufisadi wakati alipokuwa rais.


Mahakama ilikuwa na jukumu la kuamua kama Bw.Zuma anapaswa kuadhibiwa kwa kukataa wito wa mahakama na amri ya mahakama ya kumtaka afike mahakamani kutoa ushahidi kuhusu shutuma za rushwa wakati wa utawala wake.


Mwenyekiti wa kamati maalum ya uchunguzi wa mahakama ,Raymond Zondo ambayo imekuwa ikichunguza madai hayo aliiomba mahakama itamke kuwa rais huyo wa zamani alidharau mahakama na imhukumu kifungo cha miaka miwili.


Tangu alipojiuzulu mnamo mwaka 2018, Bwana Zuma amekuwa akifika mahakamani akikabiliwa na shutuma za ufisadi ambazo amekuwa akizikanusha.


Wafanyabiashara walishutumiwa kwa kula njama na wanasiasa kushawishi mchakato wa kufanya maamuzi ya serikali Rais huyo wa zamani alijitokeza mara moja kwenye uchunguzi wa kile kilichojulikana kama “kukamatwa kwa serikali” lakini akakataa kujitokeza baadaye.


Uchunguzi huo – ulioongozwa na Jaji Raymond Zondo – uliuliza Korti ya Katiba iingilie kati.


Haijulikani ikiwa Bw Zuma sasa atakamatwa.


Katika suala tofauti la kisheria, Bwana Zuma alikataa hatia mwezi uliopita katika kesi yake ya ufisadi iliyohusisha makubaliano ya silaha ya $ 5bn (£ 3bn) kutoka miaka ya 1990.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top