} });
 

 

Mchezaji wa Inter Milan na timu ya Taifa ya Denmark Christian Eriksen Jumamosi iliyopita alianguka uwanjani na kupoteza fahamu kwa tatizo la moyo (cardiac arrest) dakika ya 42 ya mchezo wa Euro 2020 kati ya Denmark dhidi ya Finland, tukio ambalo lilipelekea mchezo huo kuahirishwa kabla ya baadae kuendelea na Denmark kupoteza 1-0.

Eriksen kwa sasa bado yupo hospitali akipatiwa matibabu lakini anaendelea vizuri na ametumia ukurasa wake wa instagram kuwashukuru wote waliomuombea wakati alipopata matatizo.

“Asante sana kwa salamu zenu nzuri na ujumbe kutoka ulimwenguni kote, ina maana kubwa sana kwangu na familia yangu niko sawa na bado ninahitajika kupitia vipimo hospitalini lakini ninajihisi sawa na sasa nitawashangilia vijana kwenye timu ya Denmark katika mechi zijazo” - Christian Eriksen

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top