} });
 

 

Serikali ya Ethiopia imetangaza sitisho la mapigano katika jimbo la Tigray, miezi minane baada ya mzozo mbaya uliosababisha mafaa mengi, wakati maelfu ya wakazi wakikabiliwa na baa la njaa.

Sitisho hilo la mapigano huenda likatuliza hali kwenye taifa hilo la pili kwa wingi wa watu barani Afrika.

Taarifa inajiri wakati Ethiopia ikisuburi matokeo ya uchaguzi wa kitaifa ambao Waziri Mkuu Abiy Ahmed aliuelezea kama kiini cha mageuzi yaliyompelekea kushinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2019.

Taarifa ya Serikali ilitolewa na vyombo vya habari muda mfupi baada ya utawala wa mpito wa Tigray ulioteuliwa na serikali kuu kukimbia katika Mji Mkuu wa Tigray, Mekele, na kuomba sitisho la mapigano kwa sababu za kibinadamu ili misaada inayohitajika ifikishwe kwa kwa wakazi.

Wakati huo huo, wakazi wa Mekele wameshangilia kuwasili kwa vikosi vya Tigray.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top