} });
 


BARAZA Kuu la Umoja wa Mataifa hii leo limepitisha azimio la kumchagua katibu mkuu wa sasa wa Umoja huo Antonio Guterres kuongoza kwa awamu ya pili.

 

Baraza hilo limemthibitisha Guterres mwenye umri wa miaka 72  mwanadiplomasia raia wa Ureno, kuongoza tena Umoja huo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

 

Mapema mwezi huu, wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa pamoja walimuunga mkono Guterres kutetea nafasi hiyo ya ukatibu mkuu kwa awamu ya pili.

 

Baraza hilo huwa ndio kikwazo kikubwa kwenye mchakato huo, awamu mpya ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa inatarajiwa kuanza Januari Mosi mwaka 2022.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top