} });
 

 

JESHI la Polisi jijini Arusha, linamshikilia msaidizi wa kazi za ndani (house girl) ambaye jina lake limehifadhiwa, kwa tuhuma za kumuua kwa kumnyonga shingo mtoto Tifan Osward mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu, ambaye aliachwa nyumbani na msichana huyo wa kazi.

 

Taarifa iliyotolewa leo Juni 21, na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo inaeleza kuwa tukio hilo lilitokea Juni 19, 2021 katika eneo la Olasiti jijini Arusha ambapo taarifa za awali zinaonesha kwamba msichana huyo wa kazi, aliajiriwa miezi miwili iliyopita, akitokea mkoani Mara.

 

Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na Jeshi la Polisi na upelelezi utakapokamilika, jalada litapelekwa ofisi ya taifa ya mashtaka kwa uamuzi wa kisheria.

 

Aidha, ACP Masejo ameongeza kuwa wanaendelea kumshikilia binti huyo ili kujua nini kilipelekea kuchukua maamuzi hayo na kwamba upelelezi utakapokamilika jarida lake litapelekwa Ofisi ya Taifa ya mashtaka kwa uamuzi wa kisheria.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top