} });
 

 

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP),  Simon Sirro amefanya mabadiliko madogo kwa makamishna na makamanda wa Polisi watatu kwa lengo la kuongeza ufanisi kwenye mikakati ya kubaini, kuzuia na kukabiliana na uhalifu.

Taarifaimetolewa Msemaji wa Jeshi hilo,  David Misime imeeleza kuwa kamishna msaidizi wa polisi  (ACP) Joseph Konyo amehamishwa kutoka kitengo cha maadili makao makuu ya polisi Dodoma na kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma .

Kamanda Konyo anachukua nafasi ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma (ACP) Simon Maigwa ambaye anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro (ACP) Amon Kakwale amehamishwa katika kamisheni ya operesheni na mafunzo makao makuu ya polisi Dodoma.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top