} });
 

 

“Leo maeneo ya Tabata Liwiti kikosi maalum cha Polisi cha kufuatailia na kuzuia ujambazi, kilifanikiwa kufuatilia nyendo za wahalifu, na wahalifu wakabaini wanafuatilia walikuwa kwenye pikipiki, walipobaini wanafuatailiwa Polisi walianza kufyatua risasi lakini” Kamanda Muliro

“Polisi waliwakimbiza na wahalifu wakaanguka na pikipiki, wawili wakaanza kukimbia huku wakifyatua risasi na Polisi wakawajibika kujilinda wakaanza kufyatua risasi ambazo ziliwapata katika sehemu mbalimbali za miili yao wakapata majereha makubwa wakakimbizwa Hospitali baada ya muda walipoteza maisha wakafariki” Kamanda Muliro

“Mmoja wahalifu baada ya upekuzi alikutwa na silaha pisto, bunduki hiyo ilikutwa na risasi nne na eneo la tukio yaliokotwa maganda ya risasi, baada ya uchunguzi wa awali ilibainika kuwa baadhi ya wahalifu wale alikuwemo mhalifu sugu ambaye amekuwa akijihusisha na vitendo ya kijambazi muda mrefu” Kamanda Muliro

“Alivyochunguzwa anajulikana kwa jina la Said Gongwe, kumbukumbu zilionesha mhalifu huyu 1995 aliwahi kutuhumiwa kwa makosa ya unyanganyi wa kutumia silaha akafikishwa Mahakamani akafungwa miaka 30” Kamanda Muliro

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top