} });
 

 

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar-es-salaam (DAWASA) inawataarifu wananchi na wakazi wa Bagamoyo hadi Kigamboni kuwa huduma ya majisafi itakosekana kwa saa 24 kuanzia tarehe 8/6/2021 asubuhi hadi 9/6/2021.

Sababu ya kukosekana kwa maji ni matengenezo ya bomba kuu la usambazaji maji 54 linalotokea katika matenki ya chuo kikuu Ardhi eneo la Victoria na Makumbusho baada ya kupasuka.

Maeneo yatakayoathirika ni Mji wa Bagamoyo, Vijiji vya Zinga, Kerege, Mapinga, Bunju, Boko, Mivumoni, Kawe, Kinondoni, Ilala, Temeke, Uwanja wa ndege, Tegeta, kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi beach, Mlalakuwa,Mwenge, Mikocheni, Msasani, sinza, kijitonyama, oysterbay, Magomeni, Upanga, Kariakoo, katikati ya jiji (City center), Ubungo Maziwa, Kigogo, Mburahati, hospitali ya Rufaa Mhimbili, Kigamboni Navy na Ferry

DAWASA inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top