} });
 

 

Mkuu wa Mkoa wa DSM, Amos Makalla, amelitaka Jiji la Ilala kuhakikisha mradi wa machinjio ya kisasa Vingunguti unaanza kufanya kazi ifikapo Julai mosi ili lengo la kuanzishwa kwa machinjio hayo litimie.

Makalla ametoa agizo hilo wakati wa kikao cha pamoja kati yake na Madiwani pamoja na Maafisa Watendaji kata, ambapo amewataka viongozi hao kuwa mstari wa mbele kwenye usimamizi wa miradi ya maendeleo.

RC Makalla amelitaka Jiji la Ilala kuhakikisha linawapanga vizuri Wamachinga katika maeneo yao ili waweze kufanya biashara zao katika hali ya usalama na kwa mujibu wa sheria.

Pia Makalla amewaasa madiwani wa Jijini la Dar es Salaam kuepuka migongano na mivutano isiyokuwa na faida yoyote kwa wananchi na wajikite katika kujenga hoja na mipango ya kutatua kero kwa maslahi mapana ya wananchi huku akiwahakikishia wananchi kuwa Serikali imejidhatiti kuwalinda na mali zao kutokana na mafanikio makubwa yanayoendelea kupatikana katika operesheni Tokomeza Majambazi na Vibaka Dar es Salaam.

Kwa upande wa Madiwani na Maafisa watendaji kata wamemuhakikishia RC Makalla kuwa maelekezo na maagizo aliyoyatoa wameyapokea kwa mikono miwili na watayafanyia kazi kuanzia leo.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top