} });
 

 

Mbunge wa Momba Condester Michael Sichalwe ametolewa ndani ya ukumbi wa bunge ili akabadilishe mavazi yake baada ya mbunge wa Nyangw’ale, Hussein Nassor Amar kuomba muongozo wa Spika kuwa kuna baadhi ya wabunge wamevaa mavazi yasio na maadili.

Spika alimtaka mbunge Hussein Nassor Amar kumtaja mmoja ambaye amemuona ndipo alipomtaja Mbunge wa Momba Condester Michael Sichalwe ambapo Spika Ndugai alimtaka atoke ndani ya ukumbi wa bunge ili akabadilishe mavazi yake.

“Spika nasimama kwa kanuni ya  70 inayohusu mavazi ya staha kwa wabunge, kanuni imeeleza  wazi kuhusu mavazi hayo na kwa akina dada lakini humu ndani kuna wabunge wamevaa nguo ambazo hazina staha,” Amar.

Spika Ndugai alimpa nafasi Mbunge huyo kumtaja mwenzake  aliyevaa mavazi ambayo hayakuwa na staha ili iwe mfano.

“Mbunge huyo yuko hapo katika mkono wangu wa kulia, amevalia tisheti  lakini naomba umuite mbele uone suruali aliyovaa namna ilivyobana, amevaa miwani,”  Amar 

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top