} });
 


Mbunge wa Zamani, Selemani Bungara maarufu kama Bwege leo ni miongoni mwa wageni waliotembelea bunge kujionea shughuli mbalimbali za bunge. Akiwa nje ya ukumbi wa Bunge Bwege alipata nafasi ya kuzungumza na waandishi wa habari.

“Kuna tofauti ya Bunge letu na hili, wingi wao naona hakuna uchangamfu wa bunge lakini wanajitahidi kwa sababu Mama Samia amewaambia waseme wanavyotaka kusema kwa hiyo wanajitahidi wanasema, kutokana na siasa ilivyobadilika inawezekana nikaingia tena kwenye kinyang’anyiro lakini ingekuwa siasa zile nisingeingia siasa za mama ni tofauti”-Selemani Bungara

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top