![]() |
Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt.Athumani Ngenya akifungua mafunzo kwa wahariri wa vyombo vya habari yaliyofanyika jana Makao Makuu ya Shirika hilo Jijini Dar es Salaam. |
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limewataka waagizaji wa magari nje ya nchi kutokuagiza magari kwa watu binafsi badala yake watumie Makampuni yanayoaminika na kufahamika ili kuepuka kupata hasara kama gari likiwa halina ubora wa viwango unaotakiwa.
Akizungumza jana akifungua mafunzo kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari juu ya majukumu ya Shirika hilo yaliyofanyika Makao Makuu ya TBS jana Jijini DSM Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt Athuman Ngenya amesema kuwa uagizaji wa gari kupitia kampuni inayofahamika ni bora kwa maana tatizo lolote llinalohusu gari ambalo limegizwa kupitia kampuni hiyo itahusika.
“Kama ikitokea muagizaji wa gari atakuta kuna hitirafu ya gari basi kampuni aliyoitumia itahusika na matengenezo na kama muhusika hatatumia njia hiyo basi atakuwa kapata hasara kwani litakuwa limekosa viwango vinavyotakiwa” Dkt.Ngenya.
Aidha kwa upande wake Meneja wa Ukaguzi wa bidhaa zinazotoka nje ya nchi Mhandisi Said Mkwawa akizungumzia kuhusu ukaguzi wa magari yatokayo nje ya nchi amesema ukaguzi huo pia umefanikisha kukusanya kiasi cha bilioni 1.5 ambazo hapo awali wangepata asilimia 30 pekee
“Katika magari 4779 tulioyafanyia ukaguzi kuanzia mwezi aprili 15 mpaka June 08, asilimia 85 ya changamoto kubwa imejitokeza kwenye ubovu wa kashata,taa, na magurudumu kuisha muda wake”. Mhandisi Mkwawa.
Post a Comment