} });
 


MKUU wa mkoa wa Mara, Ally Hapi, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuwaamini vijana na kuwateua kwa ajili ya kufanya naye kazi katika serikali yake ya awamu ya sita.

 

Hapi ametoa kauli hiyo hii leo Juni 15, 2021, Jijini Mwanza, wakati akizungumza kwenye mkutano wa Rais Samia na vijana ambapo amemuahidi kuwa vijana wataendelea kumpa ushirikiano na kwamba yupo tayari kutumwa popote pale.

 

Rais kwa niaba ya vijana wote ambao umekwishatuteua kwenye serikali yako, tungependa kukushukuru sana kwa imani yako kubwa kwa vijana, nchi yetu wakati inapata uhuru Baba wa Taifa alikuwa na miaka 39 na Mzee Kawawa alikuwa na miaka 35 leo unazungumza na kundi lililoshiriki katika nchi yetu kuhakikisha tunapata ukombozi, amesema RC Hapi.

 

Aidha, ameongeza kuwa, “Vijana sisi tutakuunga mkono, tutakutii, tutapokea maelekezo yako, tutafanya kazi usiku na mchana popote pale utakapotupeleka kuhakikisha dhamira yako kwa vijana na kwa Tanzania inaenda kutimia, unalo jeshi la vijana nyuma yako ambao wako tayari kukusaidia kuitekeleza Ilani ya CCM“.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top