} });
 

 

Serikali ya Eswatini, imekanusha taarifa za Mfalme Mswati III, kulimbia taifa hilo la kusini mwa Africa kufuatia makabiliano ya wanajeshi na wandamanaji wanaoshikiza mageuzi nchini humo.

"Ningependa kuwahakikishia raia wa eswatini na jamii ya kimataifa kuwa Mfalme Mswati III yupo nchini na anaendelea na majukumu yake ya kujenga ufalme wa Eswatini " taarifa kutoka kwa kaimu waziri mkuu Themba Masuku, imesema.

Masuku ametoa wito wa utulivu kipindi hiki cha maandamano.

Maandamano dhidi ya mfulme Mswati III, ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 35 yalianza wikendi iliopita wandamanaji wakishinikiza mabadiliko ya katiba na kuondoka madarakani kwa Mswati III, kama njia ya kuelekea kwa demokrasia.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top