} });
 


Maelfu ya watu walilazimika kuhama makaazi yao kutokana na ghasia zilizotokea hapo jana nchini Somalia.

Katika taarifa iliyotolewa kwenye akaunti ya Twitter ya Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA), iliripotiwa kuwa shirika la kigaidi la Al-Shabaab lilifanya mashambulizi dhidi ya vikosi vya usalama na raia katika mkoa wa Mugud kaskazini na maeneo ya katikati mwa  nchi.

Katika taarifa hiyo ambayo ilieleza kuwa watu wasiopungua 31 walipoteza maisha kwenye mashambulizi hayo, pia iliandikwa,

"Maelfu ya watu walilazimika kuhama makaazi yao kwa sababu ya vurugu katika eneo hilo."

Serikali ya Somalia ililaani mashambulizi hayo na kutangaza kuwa zaidi ya wanamgambo 40 waliuawa.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top