} });
 

 

TANESCO wamewaomba radhi wateja kutokana na kukosekana kwa huduma ya ununuzi wa umeme wa luku June 7,2021 na kusababisha baadhi ya wateja kushindwa kununua umeme.

Taarifa iliyotolewa na  Ofisi ya Uhusiano TANESCO Makao Makuu  kupitia ukurasa wa Twitter imeeleza sababu ya kukosekana kwa huduma ni hitilafu iliyobainika wakati wa maboresho yanayoendelea katika mfumo wa manunuzi ya luku.

“Huduma ya mfumo wa manunuzi ya luku inatarajiwa kurejea leo, saa 12 jioni, tunaomba uvumilivu wakati wataalamu wetu wakiendelea na maboresho,” imeeleza taarifa hiyo.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top