} });
 

 

Na Faustine Gimu Galafoni - Dodoma

TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), idara huru ya Serikali Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyo kitovu cha ukuzaji na ulinzi wa haki za binadamu nchini hivi karibuni inatarajia kuendesha mafunzo ya siku mbili ya haki za binadamu na utawala bora kwa zaidi ya watumishi 500 wa sekta ya afya.

                               

Akizungumza na kitengo cha Mawasiliano cha tume hiyo jijini Dodoma

Kaimu Katibu Mtendaji Nabor  Assey  amesema  Lengo la kuendesha mafunzo hayo ni kukuza uelewa wa watumishi wa sekta ya afya kuhusu haki za binadamu na misingiya utawala bora ili waweze kutoa huduma   bora zaidi kwa wananchi.

 

Amefafanua kuwa Katika awamu hii ya kwanza Mafunzo hayo yatawahusisha watumishi walioko katika hospitali 11 zilizoko katika mikoa sita (6) ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar,ambapo yameanza Juni 17 na yakitarajiwa kuhitimimshwa Juni 25 mwaka huu.

 

Bw. Assey ametaja Mikoa na hospitali zitakazohusika katika mafunzo hayo ni: Dodoma (Hospitali ya Rufaa ya Mkoa); Dar es Salaam (Hospitali ya Amana, Temeke na Mwananyamala); Mwanza (Hospitali ya Rufaa ya Mkoa - Sekou toure, Hospitali ya Wilaya Ilemela na Nyamagana); na Lindi (Hospitali ya Rufaa ya Mkoa (Sokoine).

 

Kwa upande wa Zanzibar mafunzo yatafanyika Unguja (Hospitali ya Mnazi Mmoja) na Pemba (Hospitali ya Wilaya ya Wete na Chakechake.

 

Mafunzo hayo yatatolewa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa THBUB wa miaka mitano (2018/2019 – 2022/2023); ambao moja ya malengo yake ni kukuza haki za binadamu na misingi ya utawala bora. Utoaji wa mafunzo ya haki za binadamu na utawala kwa makundi mbalimbali ya watanzania ni mojawapo ya njia ya kufikia lengo hilo.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top