} });
 

 

Katika raundi ya 16 ya Mashindano ya 16 ya Soka ya Uropa (EURO 2020), Ubelgiji iliishinda Ureno 1-0 na kutinga robo fainali.

Ubelgiji na bingwa mtetezi Ureno walichuana katika mechi ya raundi ya 16 iliyochezwa kwenye Uwanja wa La Cartuja huko Seville, Uhispania.

Ubelgiji ilifunga goli lake la peke katika dakika ya 42 kupitia mchezaji Thorgan Hazard aliyetanguliza mkwaju kwenye nyavu Ureno kutoka nje ya eneo la hatari, na kuiweka timu yake mbele kwa 1-0.

Katika dakika zilizobaki, hakukuwa na goli lolote la ziada na Ubelgiji ilishinda mechi hiyo 1-0 na ikawa mpinzani wa Italia katika robo fainali. Mchezo wa robo fainali kati ya timu hizo utachezwa siku ya Ijumaa, Julai 2, saa 22:00 kwa saa za Uturuki (TSI) huko Munich, Ujerumani.

Kwa upande mwingine, Uholanzi na Czech zilikabiliana katika mechi nyingine ya raundi ya 16 iliyochezwa kwenye uwanja wa Puskas katika mji mkuu wa Budapest, Hungary.

Czech ilifunga goli la kwanza dakika ya 68 kwa mpira wa kona kutoka upande wa kulia kupitia Tomas Kalas  na kuipa Czech uongozi wa bao 1-0.

Katika dakika ya 80 Czech iliongezeka goli la pili kupitia Patrik Schick ambaye alifunga bao lake la 4 katika mashindano ya EURO 2020.

Baada ya ushindi huo wa 2-0, Czech itapambana na Denmark katika robo fainali. Mechi ya robo fainali kati ya timu hizo mbili itachezwa siku ya Jumamosi, Julai 3 saa 19.00 huko Baku, mji mkuu wa Azerbaijan.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top