} });
 


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limetangaza kiasi cha shilingi Milioni mbili kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa za kweli na kwa usiri mkubwa kwa Jeshi hilo kuhusu mtu anayefanya uhalifu wa kutumia silaha, lengo likiwa ni kuhakikisha mkoa huo unabaki kuwa shwari.

“Tumeamua kutangaza donge nono la zawadi ambazo tutawapatia kwa siri watakaotuletea taarifa za kweli zilizosahihi za kuwakamata katika mazingira yoyote watu wanaojihusisha na vitendo vya unyang’anyi wa kutumia silaha, na wakikamatwa pamoja na silaha zao, tutatoa milioni 2 palepale mchezo ukikamilika anapewa pesa yake hakuna mzunguko na hili ni zoezi endelevu,”  Kamanda Muliro.

Aidha, Kamanda Muliro amewataka wahalifu Jijini DSM kuchagua mambo mawili kuendelea kuingia kwenye msuguano na jeshi la polisi ama kuwa raia wema.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top