} });
 

 

Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro kupitia kwa kamanda wa polisi Amoni Kakwale, limethibitisha kufariki kwa askari wa Suma JKT Emmanuel Malya anayedaiwa kuuawa na askari mwenzake aliyekuwa naye kwenye lindo la TANESCO eneo la Moshi.

Kakwale amesema waliukuta mwili wa marehemu ukiwa na majeraha ambapo wanaendelea kumtafuta askari mwenzake aliyekimbia ambapo walikuwa wote.

“Tulifika eneo la tukio nakukuta mwili wake ukiwa na majeraha na silaha yake aina ya shortgun pump action ikiwa pembeni, baada ya uchunguzi tulibaini alikuwa na mwenzake na alikimbia na tunaendelea kumtafuta”-Kakwale RPC Kilimanjaro

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top