} });
 


Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron amepigwa kibao cha uso na kijana mmoja alipokuwa katika ziara ya kikazi nchini humo.

Video inayosambaa katika mitandao ya kijamii inamuonyesha Macron akitembea kuelekea katika sehemu waliyokuwepo wananchi ambapo kijana mmoja anaonekana akimshambulia kiongozi huyo na baadaye Maofisa Usalama walimuondoa Kiongozi huyo na kumpeleka eneo lenye usalama.

Baada ya tukio hilo video inamuonyesha Macron akirejea tena katika eneo la tukio na kuendelea kuwasalimia watu wengine.

Hadi sasa haijafahamika ni kwanini kijana huyo alifanya kitendo hicho, taarifa iliyotolewa na vyombo vya habari vya nchi hiyo inasema vijana wawili wanashikiliwa na polisi kutokana na tukio hilo.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top