} });
 

Picha hii haihusiani na habari hii

Na Imani Anyigulile - Mbeya
Wananchi wa kata ya Ifumbo wilayani Chunya mkoani Mbeya wameiomba serikali kuwaboreshea miundombinu ya barabara kutoka Mbalizi hadi Ifumbo ambayo wanaitegemea kwa usafiri.

Wakizungumza na Divine Radio FM wananchi hao wamesema kuwa, barabara hiyo imekuwa haipitiki katika kipindi cha masika hivyo wameiomba serikali kuwasaidia kuboresha katika kipindi hiki cha kiangazi.

Westoni Mpira ni diwani wa kata ya ifumbo, amesema kuwa barabara hiyo imekuwa ni ngumu kutengenezeka kutokana na kuhusisha wilaya tatu za Chunya, Songwe, na Mbeya Vijijini.

Katika hatua nyingine diwani huyo ameongeza kwa kusema kuwa kipaumbele chake ni kuhakikisha barabara ya kutoka Ifumbo hadi Chunya mjini inafanyiwa maboresho.

Kwa upande wake meneja wakala wa barabara mijini na vijijini TARURA wilayani Chunya Magala Magoti amesema kuwa kuna baadhi ya maeneo yamerekebishwa na hivyo wana mpango wa kufanya marekebisho zaidi baadhi ya maeneo hadi mwakani.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top