} });
 


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan jana Juni 15, amesema Serikali imeimarisha usimamizi wa hakimiliki za wasanii na kuanzia mwezi Disemba, 2021 wasanii wataanza kulipwa mirahaba yao kutokana na kazi zinazotumiwa kwenye Runinga, Redio na Mitandaoni.

 

“Sanaa na utamaduni, sekta hii imekuwa ikikua kwa kasi, miongoni mwa hatua tulizochukua ni kuimarisha usimamizi wa haki miliki za wasanii, nataka kuarifu vijana kuwa kuanzia Disemba mwaka huu wasanii wataanza kulipwa mirabaha yao kutokana na kazi zinazotumiwa kwenye Runinga, Redio na Mitandaoni.” – Rais Samia kwenye mkutano wa vijana Mkoani Mwanza.

 

Rais Samia amehitimisha  ziara ya siku tatu ya kikazi kwa kuhutubia vijana wa Mwanza na kuzindua meli mbili na chelezo moja  zilizokarabatiwa katika bandari mkoani humo.


soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top