} });
 

 

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ Simba SC, Barbara Gonzalez amesema ni bora kutwaa taji, lakini ukubali kufungwa.

Barbara ametoa kauli hiyo baada ya kukishuhudia kikosi cha Simba SC kikitwaa ubingwa wa ASFC jana Jumapili (Julai 25), kwa kuichapa Young Africans bao 1-0, Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

“Ikiwa ungeniuliza kati ya kufungwa na kuchukua kombe ningependa nini itokee, mimi ningesema bora kufungwa lakini tupate kombe.” amesema Barbara.

MABINGWA WA ASFC WAANZA SAFARI YA DAR ES SALAAM (+PICHA)

Kiongozi huyo alimaanisha Simba SC ikikua radhi kupotez mchezo wa Julai 03 kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Young Africans, lakini haikuwa tayari kupoteza ubingwa wa ASFC jana Jumapili.

Ushindi huo unawafanya Simba SC kutetea taji lao la Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ ambalo walitwaa msimu uliopita mjini Sumbawanga mkoani Rukwa baada ya kushinda mbele ya Namungo.

Tayari kikosi cha SImba SC kimeshawasili jijini Dar es salaam kikitokea mkoani Kigoma, na kupokelewa kwa shangwe na Mashabiki wake Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa julius Nyerere.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top