} });
 


Mshambuliaji wa Young Africans Ditram Nchimbi, huenda akajiunga na Biashara United Mara, baada ya kumaliza mkataba na ‘WANANCHI’.

Nchimbi ambaye alikua sehemu ya kikosi cha Young Africans kilichopambana dhidi ya Simba SC jana Jumapili (Julai 25), Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma, katika mchezo wa Fainali Kombe la Shirikisho, anapewa nafasi hiyo kutokana na kuwa na uzoefu wa kutosha wa kupambana uwanjani.

Biashara United Mara ambayo itaiwakilisha Tanzania kwenye Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao, tayari imeshatangaza kuwaacha wachezaji KUMI NA SABA (17), ikiwa ni sehemu ya kuanza mipango ya kuwasajili wengine kuelekea msimu ujao.

Hata hivyo mpaka sasa haijafahamika kama Nchimbi ana dili la kujiunga na klabu nyingine za Ligi Kuu Tanzania Bara, lakini Biashara United Mara inaendelea kuwa gumzo kubwa katika kuiwania saini yake.

Mshambuliaji huyo aliyejiunga na Young Africans mwaka 2019 akitokea Azam FC iliyokua imempeleka kwa mkopo Polisi Tanzania FC, amekua na wakati mgumu wa kuingia kwenye kikosi cha kwanza cha Kocha Nasrideen Mohamed Nabi, jambo ambalo linamnyima nafasi ya kusaini mkataba mpya huko Jangwani.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top