
Mtoto wa
mwaka mmoja na nusu, ameuawa na fisi ambaye pia amejeruhi watu watatu na mmoja
akiwa na hali mbaya.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Tabora, Safia Jongo amesema tukio hilo limetokea mwishoni mwa
wiki katika Kijiji Cha Kangeme wilayani Kaliua.
Akizungumzia
tukio hilo amesema limetokea usiku saa tisa kwa fisi kuvamia nyumba na
kumchukua mtoto huyo na kusababisha kifo chake.
Amesema
watu waliamua kumtafuta kwa lengo la kumuua lakini akajeruhi watatu na mmoja
hali yake ni mbaya.
Kamanda
Jongo amesema Polisi na askari wanyamapori walienda kupambana na fisi huyo na
kumuua baada ya kutumia risasi 49.
"Yaani watani zangu wanyamwezi fisi kwenda ndani kuchukua mtoto na risasi arobaini na tisa kutumika ni fisi wa kawaida au wa kinyamwezi,"ametania Kamanda Jongo ambaye ni mtani wa wanyamwezi.
Majeruhi wawili inaelezwa wanaendelea vizuri isipokuwa mmoja ambaye hali yake bado sio nzuri.
Post a Comment