} });
 

 

WATU wapatao 72 wameuawa na zaidi ya watu 800 wamekamatwa katika ghasia hizo zilizoanza kama maandamano alhamisi iliyopita kupinga kwenda jela kwa rais wa zamani wa nchi hiyo Jacob Zuma, aidha tume ya Umoja wa Afrika imelaani ghasia zinazoendelea Afrika Kusini zilizosababisha watu 72 kuuawa.

 

Waandamanaji waligeuza maandamano hayo na kuwa ghasia mwishoni mwa wiki, wakichoma moto, kufunga barabara kuu na kuvamia na kupora maduka.

Mamia ya wanajeshi yalitumwa kusitisha ghasia na uporaji Afrika Kusini kudhibiti machafuko hayo yaliyoibuka siku tano zilizopita.

 

Mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat, amelaani vikali vurugu hizo ambazo zimesababisha vifo vya raia na matukio mabaya ya uporaji wa mali ya umma na ya kibinafsi, uharibifu wa miundombinu, ikiwemo kusitishwa kwa huduma muhimu katika eneo la Kwazulu-Natal, Gauteng na maeneo mengine ya Afrika Kusini,” tume imeeleza katika taarifa yake.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top