} });
 


Polisi Mkoani Kilimanjaro wanamtafuta Mwanaume mmoja aliyesababisha mauaji ya Mke wake kutokana na ugomvi ambao ulitokea baada ya Mke huyo aitwae Fausta Silayo (22) kukataa kurudiana nae.

Kamanda wa Polisi Kilimanjaro Simon Maigwa amesema kwamba “Majirani wamesema mgogoro ulitokea baina ya wawili hao na Mwanaume alikua akilazimisha warudiane, walikua wametengana kwa muda na Mwanamke akarudi kwa Wazazi wao, huyu Mwanaume alikwenda kwao kuona kama wanaweza kusuluhisha lakini ikaonekana kwa matendo ya yule Mwanaume isingewezekana hivyo kwa hasira Mwanaume ndio akaamua kumchoma visu Mke wake”- Jeshi la Polisi

“Baada ya Mwanamke kupiga kelele Mwanaume akatorokea migombani na unajua Rombo ni mpakani mwa Kenya na Tanzania, ametorokea Kenya lakini tunaendelea kumsaka na tutamkamata kwasababu anafahamika, tunashirikiana na Interpol, Mwanamke alijeruhiwa lakini baadae akafariki”- Jeshi la Polisi

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top