} });
 


WATU 259 wamefariki dunia nchini Uingereza kutokana na aina mpya ya kirusi cha corona kiitwacho DELTA.


Kwa mujibu wa @DW_Kiswahili, watu 116 kati ya waliofariki walikuwa wamepata chanjo kamili ya corona na hilo ndilo lililozua maswali zaidi…… je, chanjo bado inatoa kinga dhidi ya kirusi cha DELTA?


Utafiti umeonesha kuwa kufikia sasa, hakuna chanjo iliyoidhinishwa kutoa kinga ya asilimia 100 dhidi ya maambukizo ya virusi vya corona tangu kuanzishwa kwa chanjo hizo ambapo Watu waliopata chanjo hasa wale wanaougua maradhi mengine bado wanakabiliwa na athari ya maambukizo.


Takwimu za shirika la PHE zinaonesha kuwa Watu 116 kati ya 118 waliofariki walikuwa na umri wa zaidi ya miaka 50.


Mtafiti wa masuala ya tiba, Peggy Riese wa kituo cha utafiti wa maambukizo cha Helmholtz anasema kuwa iwapo asilimia 100 ya idadi ya Watu imepata chanjo, basi idadi ndogo ya Watu waliopata chanjo pia wanakufa, Riese ameimbia DW kwamba hii haimaanishi kuwa chanjo hiyo sio salama lakini haitoi kinga ya asilimia 100.


Aina mpya ya virusi hutokea wakati virusi vinapobadilisha mfumo wake, amesema mtaalamu mwingine kuwa aina mpya ya virusi huenda ikatokea kwa muda na kuongeza kuwa aina hiyo mpya ya virusi itandelea kutokea hadi kubwa ya watu itakapopata chanjo.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top