} });
 


Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amepata chanjo ya kwanza ya kujikinga na ugonjwa wa corona.

Profesa Lipumba amepata chanjo hiyo Julai 22,2021 katika kliniki ya Umoja wa Mataifa zilizopo Masaki.

Akizungumza na waandishi baada ya kutoka kupata chanjo hiyo amesema amejikuta akipata nafasi hiyo kupitia mke wake, Gojina Mtenga, anayefanya kazi Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Watoto Duniani(UNICEF), Cox Bazaar nchini Bangladesh.

“Kama mlivyosikia wenzetu wa mashirika haya ya kimataifa wameruhusiwa kuanza kupata chanjo hizi pamoja na familia zao, hivyo na mimi kupitia mke wangu ndio imeniwezesha leo kuja kupata chanjo hii hapa na nilipata taarifa usiku wa jana ikinitaka nifike hapa leo saa tano asubuhi nashukuru kwa kulikamisha hili, “ Profesa Lipumba.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top