} });
 


Lori la mizigo No.T 887 CWN lililokuwa likitokea Dar es Salaam - Tunduma limewaka moto na kuteketea likiwa kwenye mizani ya Mpemba mjini Tunduma mkoani Songwe.

Dereva na utingo wake wamenusurika kifo katika ajali hiyo wakati wakipambana kusogeza gari mbali na mitambo ya mizani ili Kuepusha madhara makubwa zaidi

Mashuhuda na waokoaji wamesema Licha ya kuukabiri moto, kikosi kimechelewa kupokea mawasiliano kwa wakati ili kunusuru janga hilo na kwamba magari 2 ya zimamoto yamefika saa 12 eneo la tukio wakati ajali imetokea saa 10 alfajiri.

Chanzo cha moto Huo bado hakijafahamika. 

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top